Mika 6:4
Micah 6:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nimewatoa kutoka Misri na kuwakomboa kutoka nchi ya utumwa. Nilimtuma Mose awaongoze, pia Aroni na Miriamu.
Micah 6:4 in English
Micah 6:4 · Berean Standard Bible
For I brought you up from the land of Egypt and redeemed you from the house of slavery. I sent Moses before you, as well as Aaron and Miriam.
Context
2Sikilizeni, ee milima, mashtaka ya Bwana,
sikilizeni, enyi misingi ya milele ya dunia.
Kwa kuwa Bwana ana shauri dhidi ya watu wake;
anatoa mashtaka dhidi ya Israeli. 3“Watu wangu, nimewatendea nini?
Nimewalemea kwa jinsi gani? Mnijibu. 4Nimewatoa kutoka Misri na kuwakomboa
kutoka nchi ya utumwa.
Nilimtuma Mose awaongoze,
pia Aroni na Miriamu. 5Watu wangu, kumbukeni jinsi Balaki mfalme wa Moabu
alivyofanya shauri
na kile Balaamu mwana wa Beori alichojibu.
Kumbukeni safari yenu kutoka Shitimu mpaka Gilgali,
ili mfahamu matendo ya haki ya Bwana.” 6Nimjie Bwana na kitu gani na kusujudu
mbele za Mungu aliyetukuka?
Je, nije mbele zake na sadaka za kuteketezwa,
nije na ndama za mwaka mmoja?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.