Native Bible

Micah 6:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Watu wangu, nimewatendea nini? Nimewalemea kwa jinsi gani? Mnijibu.

Micah 6:3 in English

Micah 6:3 · Berean Standard Bible

‘My people, what have I done to you? Testify against Me how I have wearied you!

Context

1Sikiliza asemalo Bwana: “Simama, tetea shauri lako mbele ya milima; vilima na visikie lile unalotaka kusema. 2Sikilizeni, ee milima, mashtaka ya Bwana, sikilizeni, enyi misingi ya milele ya dunia. Kwa kuwa Bwana ana shauri dhidi ya watu wake; anatoa mashtaka dhidi ya Israeli. 3“Watu wangu, nimewatendea nini? Nimewalemea kwa jinsi gani? Mnijibu. 4Nimewatoa kutoka Misri na kuwakomboa kutoka nchi ya utumwa. Nilimtuma Mose awaongoze, pia Aroni na Miriamu. 5Watu wangu, kumbukeni jinsi Balaki mfalme wa Moabu alivyofanya shauri na kile Balaamu mwana wa Beori alichojibu. Kumbukeni safari yenu kutoka Shitimu mpaka Gilgali, ili mfahamu matendo ya haki ya Bwana.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.