Mika 3:8
Micah 3:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini kuhusu mimi, nimejazwa nguvu, nimejazwa Roho wa Bwana, haki na uweza, kumtangazia Yakobo kosa lake, na Israeli dhambi yake.
Micah 3:8 in English
Micah 3:8 · Berean Standard Bible
As for me, however, I am filled with power by the Spirit of the LORD, with justice and courage, to declare to Jacob his transgression and to Israel his sin.
Context
6Kwa hiyo usiku utawajieni, msiweze kuwa na maono,
na giza, msiweze kubashiri.
Jua litawachwea manabii hao,
nao mchana utakuwa giza kwao. 7Waonaji wataaibika
na waaguzi watafedheheka.
Wote watafunika nyuso zao
kwa sababu hakuna jibu litokalo kwa Mungu.” 8Lakini kuhusu mimi, nimejazwa nguvu,
nimejazwa Roho wa Bwana,
haki na uweza,
kumtangazia Yakobo kosa lake,
na Israeli dhambi yake. 9Sikieni hili, enyi viongozi wa nyumba ya Yakobo,
enyi watawala wa nyumba ya Israeli,
mnaodharau haki
na kupotosha kila lililo sawa; 10mnaojenga Sayuni kwa kumwaga damu
na Yerusalemu kwa uovu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.