Mika 3:10
Micah 3:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
mnaojenga Sayuni kwa kumwaga damu na Yerusalemu kwa uovu.
Micah 3:10 in English
Micah 3:10 · Berean Standard Bible
who build Zion with bloodshed and Jerusalem with iniquity.
Context
8Lakini kuhusu mimi, nimejazwa nguvu,
nimejazwa Roho wa Bwana,
haki na uweza,
kumtangazia Yakobo kosa lake,
na Israeli dhambi yake. 9Sikieni hili, enyi viongozi wa nyumba ya Yakobo,
enyi watawala wa nyumba ya Israeli,
mnaodharau haki
na kupotosha kila lililo sawa; 10mnaojenga Sayuni kwa kumwaga damu
na Yerusalemu kwa uovu. 11Viongozi wake wanahukumu kwa rushwa,
na makuhani wake wanafundisha kwa malipo,
nao manabii wake wanatabiri kwa fedha.
Hata hivyo wanamwegemea Bwana na kusema,
“Je, Bwana si yumo miongoni mwetu?
Hakuna maafa yatakayotupata.” 12Kwa hiyo kwa sababu yenu,
Sayuni italimwa kama shamba,
Yerusalemu itakuwa lundo la kokoto,
na kilima cha Hekalu
kitakuwa kichuguu
kilichofunikwa na vichaka.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.