Mathayo 8:15
Matthew 8:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akamgusa mkono wake na homa ikamwacha, naye akainuka na kuanza kumhudumia.
Matthew 8:15 in English
Matthew 8:15 · Berean Standard Bible
So He touched her hand, and the fever left her, and she got up and began to serve them.
Context
13Kisha Yesu akamwambia yule jemadari, “Nenda na iwe kwako sawasawa na imani yako.” Naye yule mtumishi akapona saa ile ile. 14Yesu alipoingia nyumbani kwa Petro, alimkuta mama mkwe wa Petro amelala kitandani, akiwa ana homa. 15Akamgusa mkono wake na homa ikamwacha, naye akainuka na kuanza kumhudumia. 16Jioni ile, wakamletea watu wengi waliopagawa na pepo wachafu, naye akawatoa wale pepo wachafu kwa neno lake, na kuwaponya wagonjwa wote. 17Haya yalifanyika ili litimie lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Isaya kwamba:
“Mwenyewe alitwaa udhaifu wetu
na alichukua magonjwa yetu.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.