Mathayo 8:16
Matthew 8:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Jioni ile, wakamletea watu wengi waliopagawa na pepo wachafu, naye akawatoa wale pepo wachafu kwa neno lake, na kuwaponya wagonjwa wote.
Matthew 8:16 in English
Matthew 8:16 · Berean Standard Bible
When evening came, many who were demon-possessed were brought to Jesus, and He drove out the spirits with a word and healed all the sick.
Context
14Yesu alipoingia nyumbani kwa Petro, alimkuta mama mkwe wa Petro amelala kitandani, akiwa ana homa. 15Akamgusa mkono wake na homa ikamwacha, naye akainuka na kuanza kumhudumia. 16Jioni ile, wakamletea watu wengi waliopagawa na pepo wachafu, naye akawatoa wale pepo wachafu kwa neno lake, na kuwaponya wagonjwa wote. 17Haya yalifanyika ili litimie lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Isaya kwamba:
“Mwenyewe alitwaa udhaifu wetu
na alichukua magonjwa yetu.” 18Yesu alipoona makutano mengi wamemzunguka, aliwaamuru wanafunzi wake wavuke mpaka ngʼambo ya ziwa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.