Mathayo 4:11
Matthew 4:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo ibilisi akamwacha, nao malaika wakaja na kumhudumia.
Matthew 4:11 in English
Matthew 4:11 · Berean Standard Bible
Then the devil left Him, and angels came and ministered to Him.
Context
9kisha akamwambia, “Nitakupa hivi vyote kama ukinisujudia na kuniabudu.” 10Yesu akamwambia, “Ondoka mbele yangu, Shetani! Kwa maana imeandikwa, ‘Mwabudu Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.’ ” 11Ndipo ibilisi akamwacha, nao malaika wakaja na kumhudumia. 12Yesu aliposikia kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa ametiwa gerezani, alirudi Galilaya. 13Akaondoka Nazareti akaenda kuishi Kapernaumu, mji ulioko karibu na bahari, katika mipaka ya nchi ya Zabuloni na Naftali,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.