Mathayo 3:5
Matthew 3:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Watu walikuwa wakimwendea kutoka Yerusalemu, Uyahudi yote na nchi zote za kandokando ya Mto Yordani.
Matthew 3:5 in English
Matthew 3:5 · Berean Standard Bible
People went out to him from Jerusalem and all Judea and the whole region around the Jordan.
Context
3Huyu ndiye yule aliyenenwa habari zake na nabii Isaya aliposema:
“Sauti ya mtu aliaye huko nyikani,
‘Tayarisheni njia kwa ajili ya Bwana,
yanyoosheni mapito yake.’ ” 4Basi Yohana alivaa mavazi yaliyotengenezwa kwa singa za ngamia, akiwa na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu. 5Watu walikuwa wakimwendea kutoka Yerusalemu, Uyahudi yote na nchi zote za kandokando ya Mto Yordani. 6Nao wakaziungama dhambi zao, akawabatiza katika Mto Yordani. 7Lakini alipowaona Mafarisayo na Masadukayo wengi wakija ili kubatizwa, aliwaambia: “Ninyi watoto wa nyoka! Ni nani aliyewaonya kuikimbia ghadhabu inayokuja?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.