Native Bible

Matthew 27:48 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ghafula mmoja wao akaenda mbio na kuleta sifongo, akaichovya kwenye siki, akaiweka kwenye mwanzi na akampa Yesu ili anywe.

Matthew 27:48 in English

Matthew 27:48 · Berean Standard Bible

One of them quickly ran and brought a sponge. He filled it with sour wine,* put it on a reed, and held it up for Jesus to drink.*

Context

46Ilipofika saa tisa, Yesu akapaza sauti akalia, “Eloi, Eloi, lama sabakthani?” (maana yake, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”) 47Baadhi ya watu waliokuwa wamesimama pale waliposikia hayo, wakasema, “Anamwita Eliya.” 48Ghafula mmoja wao akaenda mbio na kuleta sifongo, akaichovya kwenye siki, akaiweka kwenye mwanzi na akampa Yesu ili anywe. 49Wengine wakasema, “Basi mwacheni. Hebu tuone kama Eliya atakuja kumwokoa.” 50Yesu alipolia tena kwa sauti kuu, akaitoa roho yake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.