Native Bible

Matthew 27:28 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wakamvua nguo zake na kumvika vazi la rangi nyekundu, kisha

Matthew 27:28 in English

Matthew 27:28 · Berean Standard Bible

They stripped Him and put a scarlet robe on Him.

Context

26Basi akawafungulia Baraba. Lakini baada ya kuamuru Yesu achapwe mijeledi, akamtoa ili asulubishwe. 27Kisha askari wa mtawala wakampeleka Yesu kwenye Praitorio* na wakakusanya kikosi kizima cha askari kumzunguka. 28Wakamvua nguo zake na kumvika vazi la rangi nyekundu, kisha 29wakasokota taji ya miiba, wakaiweka kichwani pake. Wakamwekea fimbo katika mkono wake wa kuume, na wakapiga magoti mbele zake na kumdhihaki, wakisema, “Salamu, mfalme wa Wayahudi!” 30Wakamtemea mate, wakachukua ile fimbo wakampiga kichwani tena na tena.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.