Mathayo 21:9
Matthew 21:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ule umati wa watu uliomtangulia na ule uliomfuata ukapiga kelele ukisema, “Hosana,* Mwana wa Daudi!” “Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!” “Hosana juu mbinguni!”
Matthew 21:9 in English
Matthew 21:9 · Berean Standard Bible
The crowds that went ahead of Him and those that followed were shouting: “Hosanna to the Son of David!”* “Blessed is He who comes in the name of the Lord!”* “Hosanna in the highest!”*
Context
7Wakamleta yule punda na mwana-punda, nao wakatandika mavazi yao juu ya hao punda, naye Yesu akaketi juu yake. 8Umati mkubwa wa watu ukatandaza mavazi yao barabarani, na wengine wakakata matawi kutoka kwenye miti, wakayatandaza barabarani. 9Ule umati wa watu uliomtangulia na ule uliomfuata ukapiga kelele ukisema,
“Hosana,* Mwana wa Daudi!”
“Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!”
“Hosana juu mbinguni!” 10Yesu alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakauliza, “Huyu ni nani?” 11Ule umati wa watu ukajibu, “Huyu ni Yesu, yule nabii kutoka Nazareti katika Galilaya.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.