Mathayo 21:8
Matthew 21:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Umati mkubwa wa watu ukatandaza mavazi yao barabarani, na wengine wakakata matawi kutoka kwenye miti, wakayatandaza barabarani.
Matthew 21:8 in English
Matthew 21:8 · Berean Standard Bible
A massive crowd spread their cloaks on the road, while others cut branches from the trees and spread them on the road.
Context
6Wale wanafunzi wakaenda, wakafanya kama Yesu alivyokuwa amewaagiza. 7Wakamleta yule punda na mwana-punda, nao wakatandika mavazi yao juu ya hao punda, naye Yesu akaketi juu yake. 8Umati mkubwa wa watu ukatandaza mavazi yao barabarani, na wengine wakakata matawi kutoka kwenye miti, wakayatandaza barabarani. 9Ule umati wa watu uliomtangulia na ule uliomfuata ukapiga kelele ukisema,
“Hosana,* Mwana wa Daudi!”
“Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!”
“Hosana juu mbinguni!” 10Yesu alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakauliza, “Huyu ni nani?”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.