Mathayo 21:11
Matthew 21:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ule umati wa watu ukajibu, “Huyu ni Yesu, yule nabii kutoka Nazareti katika Galilaya.”
Matthew 21:11 in English
Matthew 21:11 · Berean Standard Bible
The crowds replied, “This is Jesus, the prophet from Nazareth in Galilee.”
Context
9Ule umati wa watu uliomtangulia na ule uliomfuata ukapiga kelele ukisema,
“Hosana,* Mwana wa Daudi!”
“Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!”
“Hosana juu mbinguni!” 10Yesu alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakauliza, “Huyu ni nani?” 11Ule umati wa watu ukajibu, “Huyu ni Yesu, yule nabii kutoka Nazareti katika Galilaya.” 12Yesu akaingia katika eneo la Hekalu na kuwafukuza wote waliokuwa wakinunua na kuuza vitu Hekaluni. Akazipindua meza za wale waliokuwa wakibadilisha fedha, na pia viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa. 13Akawaambia, “Imeandikwa, ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala,’ lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyangʼanyi.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.