Native Bible

Matthew 20:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Akawaambia, ‘Ninyi nanyi nendeni mkafanye kazi katika shamba langu la mizabibu, nami nitawalipa chochote kilicho haki yenu.’

Matthew 20:4 in English

Matthew 20:4 · Berean Standard Bible

‘You also go into my vineyard,’ he said, ‘and I will pay you whatever is right.’

Context

2Baada ya kukubaliana na hao vibarua kuwalipa ujira wa dinari* moja kwa siku, akawapeleka kwenye shamba lake la mizabibu. 3“Mnamo saa tatu akatoka tena, akawakuta wengine wamesimama sokoni bila kazi. 4Akawaambia, ‘Ninyi nanyi nendeni mkafanye kazi katika shamba langu la mizabibu, nami nitawalipa chochote kilicho haki yenu.’ 5Kwa hiyo wakaenda. “Akatoka tena mnamo saa sita na pia saa tisa akafanya vivyo hivyo. 6Mnamo saa kumi na moja akatoka tena akawakuta wengine bado wamesimama bila kazi. Akawauliza, ‘Kwa nini mmesimama hapa kutwa nzima pasipo kufanya kazi?’

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.