Mathayo 20:32
Matthew 20:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yesu akasimama na kuwaita, akawauliza, “Mnataka niwafanyie nini?”
Matthew 20:32 in English
Matthew 20:32 · Berean Standard Bible
Jesus stopped and called them. “What do you want Me to do for you?” He asked.
Context
30Vipofu wawili walikuwa wameketi kando ya barabara. Waliposikia kwamba Yesu alikuwa anapita, wakapiga kelele wakisema, “Bwana, Mwana wa Daudi, tuhurumie!” 31Ule umati wa watu ukawakemea na kuwaambia wanyamaze, lakini wao wakazidi kupaza sauti, wakisema, “Bwana, Mwana wa Daudi, tuhurumie.” 32Yesu akasimama na kuwaita, akawauliza, “Mnataka niwafanyie nini?” 33Wakamjibu, “Bwana, tunataka kuona.” 34Yesu akawahurumia na kuwagusa macho yao. Mara macho yao yakapata kuona, nao wakamfuata.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.