Mathayo 18:29
Matthew 18:29 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Yule mtumishi mwenzake akapiga magoti akamsihi akisema, ‘Naomba univumilie, nami nitakulipa deni lako lote.’
Matthew 18:29 in English
Matthew 18:29 · Berean Standard Bible
So his fellow servant fell down and begged him, ‘Have patience with me, and I will pay you back.’
Context
27Yule bwana wa huyo mtumishi akamwonea huruma, akafuta deni lake lote, akamwacha aende zake. 28“Lakini yule mtumishi alipokuwa anatoka nje, akakutana na mtumishi mwenzake aliyekuwa amemkopesha dinari* mia moja. Akamkamata, akamkaba koo akimwambia, ‘Nilipe kile ninachokudai!’ 29“Yule mtumishi mwenzake akapiga magoti akamsihi akisema, ‘Naomba univumilie, nami nitakulipa deni lako lote.’ 30“Lakini akakataa. Badala yake, alienda akamtupa gerezani hata atakapolipa hilo deni. 31Watumishi wenzake walipoona haya yaliyotukia wakaudhika sana, nao wakaenda na kumwambia bwana wao kila kitu kilichokuwa kimetukia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.