Mathayo 18:31
Matthew 18:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Watumishi wenzake walipoona haya yaliyotukia wakaudhika sana, nao wakaenda na kumwambia bwana wao kila kitu kilichokuwa kimetukia.
Matthew 18:31 in English
Matthew 18:31 · Berean Standard Bible
When his fellow servants saw what had happened, they were greatly distressed, and they went and recounted all of this to their master.
Context
29“Yule mtumishi mwenzake akapiga magoti akamsihi akisema, ‘Naomba univumilie, nami nitakulipa deni lako lote.’ 30“Lakini akakataa. Badala yake, alienda akamtupa gerezani hata atakapolipa hilo deni. 31Watumishi wenzake walipoona haya yaliyotukia wakaudhika sana, nao wakaenda na kumwambia bwana wao kila kitu kilichokuwa kimetukia. 32“Yule bwana akamwita yule mtumishi akamwambia, ‘Wewe mtumishi mwovu! Mimi nilikusamehe deni lako lote uliponisihi. 33Je, haikukupasa kumhurumia mtumishi mwenzako kama mimi nilivyokuhurumia wewe?’
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.