Mathayo 14:3
Matthew 14:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Herode alikuwa amemkamata Yohana, akamfunga na kumweka gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, ndugu yake,
Matthew 14:3 in English
Matthew 14:3 · Berean Standard Bible
Now Herod had arrested John and bound him and put him in prison on account of Herodias, his brother Philip’s wife,
Context
1Wakati huo, Mfalme Herode, mtawala wa Galilaya, alisikia habari za Yesu, 2akawaambia watumishi wake, “Huyu ni Yohana Mbatizaji; amefufuka kutoka kwa wafu! Hii ndiyo sababu nguvu za kutenda miujiza zinafanya kazi ndani yake.” 3Herode alikuwa amemkamata Yohana, akamfunga na kumweka gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, ndugu yake, 4kwa kuwa Yohana alikuwa amemwambia Herode: “Si halali kwako kuwa na huyo mwanamke.” 5Herode alitaka sana kumuua Yohana, lakini akaogopa watu, kwa maana walimtambua kuwa ni nabii.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.