Mathayo 14:5
Matthew 14:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Herode alitaka sana kumuua Yohana, lakini akaogopa watu, kwa maana walimtambua kuwa ni nabii.
Matthew 14:5 in English
Matthew 14:5 · Berean Standard Bible
Although Herod wanted to kill John, he was afraid of the people, because they regarded John as a prophet.
Context
3Herode alikuwa amemkamata Yohana, akamfunga na kumweka gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, ndugu yake, 4kwa kuwa Yohana alikuwa amemwambia Herode: “Si halali kwako kuwa na huyo mwanamke.” 5Herode alitaka sana kumuua Yohana, lakini akaogopa watu, kwa maana walimtambua kuwa ni nabii. 6Katika siku ya kuadhimisha sikukuu ya kuzaliwa kwa Herode, binti wa Herodia alicheza mbele ya watu waliohudhuria, akamfurahisha sana Herode, 7kiasi kwamba aliahidi kwa kiapo kumpa huyo binti chochote angeomba.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.