Mathayo 13:37
Matthew 13:37 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Akawaambia, “Aliyepanda mbegu nzuri ni Mwana wa Adamu.
Matthew 13:37 in English
Matthew 13:37 · Berean Standard Bible
He replied, “The One who sows the good seed is the Son of Man.
Context
35Hii ilikuwa ili kutimiza lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii aliposema:
“Nitafungua kinywa changu niseme nao kwa mifano;
nitahubiri mambo yaliyofichika
tangu kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu.” 36Kisha Yesu akaagana na makutano, akaingia nyumbani. Wanafunzi wake wakamjia wakamwambia, “Tueleze maana ya ule mfano wa magugu shambani.” 37Akawaambia, “Aliyepanda mbegu nzuri ni Mwana wa Adamu. 38Shamba ni ulimwengu na mbegu nzuri ni wana wa Ufalme. Magugu ni wana wa yule mwovu. 39Yule adui aliyepanda magugu ni ibilisi. Mavuno ni mwisho wa dunia, nao wavunaji ni malaika.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.