Mathayo 13:16
Matthew 13:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini heri macho yenu kwa sababu yanaona, na heri masikio yenu kwa sababu yanasikia.
Matthew 13:16 in English
Matthew 13:16 · Berean Standard Bible
But blessed are your eyes because they see, and your ears because they hear.
Context
14Kwao unatimia ule unabii wa Isaya aliposema:
“ ‘Hakika mtasikiliza lakini hamtaelewa;
na pia mtatazama lakini hamtaona. 15Kwa kuwa mioyo ya watu hawa imekuwa migumu;
hawasikii kwa masikio yao,
na wamefumba macho yao.
Wasije wakaona kwa macho yao,
na wakasikiliza kwa masikio yao,
wakaelewa kwa mioyo yao,
na kugeuka nami nikawaponya.’ 16Lakini heri macho yenu kwa sababu yanaona, na heri masikio yenu kwa sababu yanasikia. 17Amin, nawaambia, manabii wengi na wenye haki walitamani kuona yale mnayoyaona lakini hawakuyaona, na walitamani kusikia yale mnayoyasikia lakini hawakuyasikia. 18“Sikilizeni basi maana ya ule mfano wa mpanzi:
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.