Native Bible

Matthew 13:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Sikilizeni basi maana ya ule mfano wa mpanzi:

Matthew 13:18 in English

Matthew 13:18 · Berean Standard Bible

Consider, then, the parable of the sower:

Context

16Lakini heri macho yenu kwa sababu yanaona, na heri masikio yenu kwa sababu yanasikia. 17Amin, nawaambia, manabii wengi na wenye haki walitamani kuona yale mnayoyaona lakini hawakuyaona, na walitamani kusikia yale mnayoyasikia lakini hawakuyasikia. 18“Sikilizeni basi maana ya ule mfano wa mpanzi: 19Mtu yeyote anaposikia neno la Ufalme naye asilielewe, yule mwovu huja na kunyakua kile kilichopandwa moyoni mwake. Hii ndiyo ile mbegu iliyopandwa kando ya njia. 20Ile mbegu iliyopandwa kwenye sehemu yenye mawe ni mtu yule ambaye hulisikia neno na mara hulipokea kwa furaha.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.