Mathayo 1:21
Matthew 1:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Naye atamzaa mwana, nawe utamwita Jina lake Yesu,* kwa maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka dhambi zao.”
Matthew 1:21 in English
Matthew 1:21 · Berean Standard Bible
She will give birth to a Son, and you are to give Him the name Jesus,* because He will save His people from their sins.”
Context
19Kwa kuwa Yosefu, mwanaume aliyekuwa amemposa alikuwa mtu mwadilifu, hakutaka kumwaibisha Maria hadharani, aliazimu kumwacha kwa siri. 20Lakini mara alipoazimu kufanya jambo hili, malaika wa Bwana akamtokea katika ndoto na kusema, “Yosefu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Maria awe mke wako, kwa maana mimba aliyo nayo ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 21Naye atamzaa mwana, nawe utamwita Jina lake Yesu,* kwa maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka dhambi zao.” 22Haya yote yalitukia ili litimie lile Bwana alilokuwa amenena kupitia nabii, akisema: 23“Tazama, bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana, nao watamwita Jina lake Imanueli”: maana yake, “Mungu pamoja nasi.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.