Native Bible

Luke 3:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yohana akawajibu akawaambia, “Mimi nawabatiza kwa maji.* Lakini atakuja aliye na nguvu kuniliko mimi, ambaye sistahili hata kufungua kamba za viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.

Luke 3:16 in English

Luke 3:16 · Berean Standard Bible

John answered all of them: “I baptize you with water,* but One more powerful than I will come, the straps of whose sandals I am not worthy to untie.* He will baptize you with the Holy Spirit and with fire.*

Context

14Askari nao wakamuuliza, “Je, nasi inatupasa tufanye nini?” Akawaambia, “Msimdhulumu mtu wala msimshtaki mtu kwa uongo, bali mridhike na mishahara yenu.” 15Watu walikuwa na matazamio makubwa. Wakawa wanajiuliza mioyoni mwao iwapo Yohana angeweza kuwa ndiye Kristo.* 16Yohana akawajibu akawaambia, “Mimi nawabatiza kwa maji.* Lakini atakuja aliye na nguvu kuniliko mimi, ambaye sistahili hata kufungua kamba za viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. 17Pepeto lake liko mkononi, tayari kusafisha sakafu yake ya kupuria na kuikusanya ngano ghalani, lakini makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.” 18Basi, kwa maonyo mengine mengi Yohana aliwasihi na kuwahubiria watu Habari Njema.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.