Native Bible

Luke 3:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Basi, kwa maonyo mengine mengi Yohana aliwasihi na kuwahubiria watu Habari Njema.

Luke 3:18 in English

Luke 3:18 · Berean Standard Bible

With these and many other exhortations, John proclaimed the good news to the people.

Context

16Yohana akawajibu akawaambia, “Mimi nawabatiza kwa maji.* Lakini atakuja aliye na nguvu kuniliko mimi, ambaye sistahili hata kufungua kamba za viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. 17Pepeto lake liko mkononi, tayari kusafisha sakafu yake ya kupuria na kuikusanya ngano ghalani, lakini makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.” 18Basi, kwa maonyo mengine mengi Yohana aliwasihi na kuwahubiria watu Habari Njema. 19Lakini Yohana alipomkemea Mfalme Herode kuhusu uhusiano wake na Herodia, mke wa ndugu yake, na maovu mengine aliyokuwa amefanya, 20Herode aliongezea jambo hili kwa hayo mengine yote: alimfunga Yohana gerezani.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.