Native Bible

Luke 3:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Watu walikuwa na matazamio makubwa. Wakawa wanajiuliza mioyoni mwao iwapo Yohana angeweza kuwa ndiye Kristo.*

Luke 3:15 in English

Luke 3:15 · Berean Standard Bible

The people were waiting expectantly and were all wondering in their hearts if John could be the Christ.

Context

13Akawaambia, “Msichukue zaidi ya kiwango mlichopangiwa.” 14Askari nao wakamuuliza, “Je, nasi inatupasa tufanye nini?” Akawaambia, “Msimdhulumu mtu wala msimshtaki mtu kwa uongo, bali mridhike na mishahara yenu.” 15Watu walikuwa na matazamio makubwa. Wakawa wanajiuliza mioyoni mwao iwapo Yohana angeweza kuwa ndiye Kristo.* 16Yohana akawajibu akawaambia, “Mimi nawabatiza kwa maji.* Lakini atakuja aliye na nguvu kuniliko mimi, ambaye sistahili hata kufungua kamba za viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. 17Pepeto lake liko mkononi, tayari kusafisha sakafu yake ya kupuria na kuikusanya ngano ghalani, lakini makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.