Luka 24:3
Luke 24:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
lakini walipoingia ndani, hawakuuona mwili wa Bwana Yesu.
Luke 24:3 in English
Luke 24:3 · Berean Standard Bible
but when they entered, they did not find the body of the Lord Jesus.
Context
1Mnamo siku ya kwanza ya juma, alfajiri na mapema, wale wanawake walichukua yale manukato waliyokuwa wameyaandaa, wakaenda kaburini. 2Wakakuta lile jiwe limevingirishwa kutoka kwenye kaburi, 3lakini walipoingia ndani, hawakuuona mwili wa Bwana Yesu. 4Walipokuwa wanashangaa juu ya jambo hili, ghafula watu wawili waliokuwa wamevaa mavazi yanayongʼaa kama umeme wakasimama karibu nao. 5Wale wanawake, wakiwa na hofu, wakainamisha nyuso zao mpaka chini. Lakini wale watu wakawaambia, “Kwa nini mnamtafuta aliye hai miongoni mwa wafu?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.