Luka 24:27
Luke 24:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Naye akianzia na Sheria ya Mose na Manabii wote, akawafafanulia jinsi Maandiko yalivyosema kumhusu yeye.
Luke 24:27 in English
Luke 24:27 · Berean Standard Bible
And beginning with Moses and all the Prophets, He explained to them what was written in all the Scriptures about Himself.
Context
25Yesu akawaambia, “Ninyi ni wajinga kiasi gani, nanyi ni wazito mioyoni mwenu kuamini mambo yote yaliyonenwa na manabii! 26Je, haikumpasa Kristo* kuteswa kwa njia hiyo na kisha aingie katika utukufu wake?” 27Naye akianzia na Sheria ya Mose na Manabii wote, akawafafanulia jinsi Maandiko yalivyosema kumhusu yeye. 28Nao walipokaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, Yesu akawa kama anaendelea mbele. 29Lakini wao wakamsihi sana akae nao, wakisema, “Kaa hapa nasi, kwa maana sasa ni jioni na usiku unaingia.” Basi akaingia ndani kukaa nao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.