Luka 24:28
Luke 24:28 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nao walipokaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, Yesu akawa kama anaendelea mbele.
Luke 24:28 in English
Luke 24:28 · Berean Standard Bible
As they approached the village where they were headed, He seemed to be going farther.
Context
26Je, haikumpasa Kristo* kuteswa kwa njia hiyo na kisha aingie katika utukufu wake?” 27Naye akianzia na Sheria ya Mose na Manabii wote, akawafafanulia jinsi Maandiko yalivyosema kumhusu yeye. 28Nao walipokaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, Yesu akawa kama anaendelea mbele. 29Lakini wao wakamsihi sana akae nao, wakisema, “Kaa hapa nasi, kwa maana sasa ni jioni na usiku unaingia.” Basi akaingia ndani kukaa nao. 30Alipokuwa mezani pamoja nao, akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akaanza kuwagawia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.