Luka 23:38
Luke 23:38 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwenye msalaba juu ya kichwa chake, kulikuwa na maandishi haya: Huyu ndiye Mfalme wa Wayahudi. Maandishi haya yalikuwa yameandikwa kwa lugha za Kiyunani, Kilatini na Kiebrania.
Luke 23:38 in English
Luke 23:38 · Berean Standard Bible
Above Him was posted an inscription:* THIS IS THE KING OF THE JEWS.
Context
36Askari nao wakaja, wakamdhihaki. Wakamletea siki ili anywe, 37na wakamwambia, “Kama wewe ni Mfalme wa Wayahudi, jiokoe mwenyewe.” 38Kwenye msalaba juu ya kichwa chake, kulikuwa na maandishi haya: Huyu ndiye Mfalme wa Wayahudi.
Maandishi haya yalikuwa yameandikwa kwa lugha za Kiyunani, Kilatini na Kiebrania. 39Mmoja wa wale wahalifu waliosulubiwa pamoja naye akamtukana, akasema: “Wewe si ndiye Kristo? Jiokoe mwenyewe na utuokoe na sisi.” 40Lakini yule mhalifu mwingine akamkemea mwenzake, akasema, “Je, wewe humwogopi Mungu, wakati uko kwenye adhabu iyo hiyo?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.