Native Bible

Luke 23:37 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

na wakamwambia, “Kama wewe ni Mfalme wa Wayahudi, jiokoe mwenyewe.”

Luke 23:37 in English

Luke 23:37 · Berean Standard Bible

“If You are the King of the Jews,” they said, “save Yourself!”

Context

35Watu wakasimama hapo wakimwangalia, nao viongozi wa Wayahudi wakamdhihaki wakisema, “Aliokoa wengine! Ajiokoe mwenyewe basi, kama yeye ndiye Kristo wa Mungu, Mteule wake.” 36Askari nao wakaja, wakamdhihaki. Wakamletea siki ili anywe, 37na wakamwambia, “Kama wewe ni Mfalme wa Wayahudi, jiokoe mwenyewe.” 38Kwenye msalaba juu ya kichwa chake, kulikuwa na maandishi haya: Huyu ndiye Mfalme wa Wayahudi. Maandishi haya yalikuwa yameandikwa kwa lugha za Kiyunani, Kilatini na Kiebrania. 39Mmoja wa wale wahalifu waliosulubiwa pamoja naye akamtukana, akasema: “Wewe si ndiye Kristo? Jiokoe mwenyewe na utuokoe na sisi.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.