Luka 22:42
Luke 22:42 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
akisema, “Baba, kama ni mapenzi yako, niondolee kikombe hiki. Lakini si kama nipendavyo, bali mapenzi yako yatendeke.”
Luke 22:42 in English
Luke 22:42 · Berean Standard Bible
“Father, if You are willing, take this cup from Me. Yet not My will, but Yours be done.”
Context
40Walipofika huko, akawaambia wanafunzi wake, “Ombeni, msije mkaingia majaribuni.” 41Akajitenga nao kama umbali wa kutupa jiwe, akapiga magoti, akaomba 42akisema, “Baba, kama ni mapenzi yako, niondolee kikombe hiki. Lakini si kama nipendavyo, bali mapenzi yako yatendeke.” 43Malaika kutoka mbinguni akamtokea, akamtia nguvu. 44Naye akiwa katika maumivu makuu, akaomba kwa bidii, nalo jasho lake likawa kama matone ya damu yakidondoka ardhini.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.