Native Bible

Luke 2:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ghafula pakawa na jeshi kubwa la mbinguni pamoja na huyo malaika wakimsifu Mungu wakisema,

Luke 2:13 in English

Luke 2:13 · Berean Standard Bible

And suddenly there appeared with the angel a great multitude of the heavenly host, praising God and saying:

Context

11Leo katika mji wa Daudi kwa ajili yenu amezaliwa Mwokozi, ndiye Kristo* Bwana. 12Hii ndiyo itakayokuwa ishara kwenu: Mtamkuta mtoto mchanga amefunikwa nguo za kitoto na kulazwa katika hori ya kulia ngʼombe.” 13Ghafula pakawa na jeshi kubwa la mbinguni pamoja na huyo malaika wakimsifu Mungu wakisema, 14“Atukuzwe Mungu juu mbinguni, na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.” 15Hao malaika walipokwisha kuondoka na kwenda zao mbinguni, wale wachungaji wakasemezana wao kwa wao, “Twendeni Bethlehemu tukaone mambo haya ya ajabu yaliyotukia, ambayo Bwana ametuambia habari zake.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.