Native Bible

Luke 11:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa sababu rafiki yangu amekuja kutoka safarini, nami sina kitu cha kumpa.’

Luke 11:6 in English

Luke 11:6 · Berean Standard Bible

because a friend of mine has come to me on a journey, and I have nothing to set before him.’

Context

4Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa na sisi huwasamehe wote wanaotukosea. Wala usitutie majaribuni (bali utuokoe kutoka kwa yule mwovu).’ ” 5Kisha akawaambia, “Ni nani miongoni mwenu mwenye rafiki yake, naye akamwendea usiku wa manane na kumwambia, ‘Rafiki, nikopeshe mikate mitatu. 6Kwa sababu rafiki yangu amekuja kutoka safarini, nami sina kitu cha kumpa.’ 7“Kisha yule aliyeko ndani amjibu, ‘Usinisumbue. Mlango umefungwa, nami na watoto wangu tumelala. Siwezi kuamka nikupe chochote.’ 8Nawaambia, ingawa huyo mtu hataamka na kumpa hiyo mikate kwa sababu ni rafiki yake, lakini kwa sababu ya kuendelea kwake kuomba, ataamka na kumpa kiasi anachohitaji.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.