Luka 11:4
Luke 11:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa na sisi huwasamehe wote wanaotukosea. Wala usitutie majaribuni (bali utuokoe kutoka kwa yule mwovu).’ ”
Luke 11:4 in English
Luke 11:4 · Berean Standard Bible
And forgive us our sins, for we also forgive everyone who sins against us. And lead us not into temptation.*’”
Context
2Akawaambia, “Mnapoomba, semeni:
“ ‘Baba yetu (uliye mbinguni),
jina lako litukuzwe,
ufalme wako uje.
(Mapenzi yako yafanyike
hapa duniani kama huko mbinguni.) 3Utupatie kila siku riziki yetu. 4Utusamehe dhambi zetu,
kwa kuwa na sisi huwasamehe wote wanaotukosea.
Wala usitutie majaribuni
(bali utuokoe kutoka kwa yule mwovu).’ ” 5Kisha akawaambia, “Ni nani miongoni mwenu mwenye rafiki yake, naye akamwendea usiku wa manane na kumwambia, ‘Rafiki, nikopeshe mikate mitatu. 6Kwa sababu rafiki yangu amekuja kutoka safarini, nami sina kitu cha kumpa.’
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.