Native Bible

Luke 1:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanaume na utamwita jina lake Yesu.

Luke 1:31 in English

Luke 1:31 · Berean Standard Bible

Behold, you will conceive and give birth to a son, and you are to give Him the name Jesus.

Context

29Maria akafadhaishwa sana na maneno haya, akajiuliza moyoni, “Salamu hii ni ya namna gani?” 30Ndipo malaika akamwambia, “Usiogope, Maria, umepata kibali kwa Mungu. 31Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanaume na utamwita jina lake Yesu. 32Yeye atakuwa mkuu, naye ataitwa Mwana wa Aliye Juu Sana. Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake. 33Ataimiliki nyumba ya Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.