Native Bible

Leviticus 19:35 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“ ‘Usitumie vipimo vya udanganyifu unapopima urefu, kupima uzito, wala kupima wingi.

Leviticus 19:35 in English

Leviticus 19:35 · Berean Standard Bible

You must not use dishonest measures of length, weight, or volume.

Context

33“ ‘Wakati mgeni anaishi pamoja nawe katika nchi yako, usimnyanyase. 34Mgeni anayeishi pamoja nawe ni lazima umtendee kama mmoja wa wazawa wa nchi yako. Mpende kama unavyojipenda mwenyewe, kwa maana ulikuwa mgeni katika nchi ya Misri. Mimi ndimi Bwana Mungu wako. 35“ ‘Usitumie vipimo vya udanganyifu unapopima urefu, kupima uzito, wala kupima wingi. 36Tumia mizani halali, mawe ya kupimia uzito halali, efa* halali, na hini* halali. Mimi ndimi Bwana Mungu wako, ambaye alikutoa katika nchi ya Misri. 37“ ‘Shika amri zangu zote na sheria zangu zote, nawe uzifuate. Mimi ndimi Bwana.’ ”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.