Native Bible

Leviticus 19:34 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mgeni anayeishi pamoja nawe ni lazima umtendee kama mmoja wa wazawa wa nchi yako. Mpende kama unavyojipenda mwenyewe, kwa maana ulikuwa mgeni katika nchi ya Misri. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.

Leviticus 19:34 in English

Leviticus 19:34 · Berean Standard Bible

You must treat the foreigner living among you as native-born and love him as yourself, for you were foreigners in the land of Egypt. I am the LORD your God.

Context

32“ ‘Uwapo mbele ya mzee, simama ili kuonyesha heshima kwa wazee, nawe umche Mungu wako. Mimi ndimi Bwana. 33“ ‘Wakati mgeni anaishi pamoja nawe katika nchi yako, usimnyanyase. 34Mgeni anayeishi pamoja nawe ni lazima umtendee kama mmoja wa wazawa wa nchi yako. Mpende kama unavyojipenda mwenyewe, kwa maana ulikuwa mgeni katika nchi ya Misri. Mimi ndimi Bwana Mungu wako. 35“ ‘Usitumie vipimo vya udanganyifu unapopima urefu, kupima uzito, wala kupima wingi. 36Tumia mizani halali, mawe ya kupimia uzito halali, efa* halali, na hini* halali. Mimi ndimi Bwana Mungu wako, ambaye alikutoa katika nchi ya Misri.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.