Native Bible

Leviticus 11:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mwaweza kula mnyama yeyote mwenye kwato zilizogawanyika sehemu mbili na ambaye hucheua.

Leviticus 11:3 in English

Leviticus 11:3 · Berean Standard Bible

You may eat any animal that has a split hoof completely divided and that chews the cud.

Context

1Bwana akawaambia Mose na Aroni, 2“Waambieni Waisraeli: ‘Kati ya wanyama wote waishio juu ya nchi, hawa ndio mtakaowala: 3Mwaweza kula mnyama yeyote mwenye kwato zilizogawanyika sehemu mbili na ambaye hucheua. 4“ ‘Kuna wanyama wengine ambao hucheua tu au wenye kwato zilizogawanyika tu, lakini hao kamwe msiwale. Ngamia ingawa hucheua hana kwato zilizogawanyika; kwa kawaida ya ibada hiyo ni najisi kwenu. 5Pelele ingawa hucheua hana kwato zilizogawanyika; huyo ni najisi kwenu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.