Native Bible

Lamentations 2:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Vijana na wazee hujilaza pamoja katika mavumbi ya barabarani, wavulana wangu na wasichana wameanguka kwa upanga. Umewaua katika siku ya hasira yako, umewachinja bila huruma.

Lamentations 2:21 in English

Lamentations 2:21 · Berean Standard Bible

Both young and old lie together in the dust of the streets. My young men and maidens have fallen by the sword. You have slain them in the day of Your anger; You have slaughtered them without compassion.

Context

19Inuka, lia usiku, zamu za usiku zianzapo; mimina moyo wako kama maji mbele za Bwana. Mwinulie yeye mikono yako kwa ajili ya maisha ya watoto wako, ambao wanazimia kwa njaa kwenye kila mwanzo wa barabara. 20“Tazama, Ee Bwana, ufikirie: Ni nani ambaye umepata kumtendea namna hii? Je, wanawake wakule wazao wao, watoto waliowalea? Je, kuhani na nabii auawe mahali patakatifu pa Bwana? 21“Vijana na wazee hujilaza pamoja katika mavumbi ya barabarani, wavulana wangu na wasichana wameanguka kwa upanga. Umewaua katika siku ya hasira yako, umewachinja bila huruma. 22“Kama ulivyoita siku ya karamu, ndivyo ulivyoagiza hofu kuu dhidi yangu kila upande. Katika siku ya hasira ya Bwana hakuna yeyote aliyekwepa au kupona; wale niliowatunza na kuwalea, adui yangu amewaangamiza.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.