Maombolezo 1:10
Lamentations 1:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Adui ametia mikono juu ya hazina zake zote, aliona mataifa ya kipagani wakiingia mahali patakatifu pake, wale uliowakataza kuingia kwenye kusanyiko lako.
Lamentations 1:10 in English
Lamentations 1:10 · Berean Standard Bible
The adversary has seized all her treasures. For she has seen the nations enter her sanctuary— those You had forbidden to enter Your assembly.
Context
8Yerusalemu ametenda dhambi sana
kwa hiyo amekuwa najisi.
Wote waliomheshimu wanamdharau,
kwa maana wameuona uchi wake.
Yeye mwenyewe anapiga kite
na kugeukia mbali. 9Uchafu wake umegandamana na nguo zake;
hakuwaza juu ya maisha yake ya baadaye.
Anguko lake lilikuwa la kushangaza,
hapakuwepo na yeyote wa kumfariji.
“Tazama, Ee Bwana, teso langu,
kwa maana adui ameshinda.” 10Adui ametia mikono
juu ya hazina zake zote,
aliona mataifa ya kipagani
wakiingia mahali patakatifu pake,
wale uliowakataza kuingia
kwenye kusanyiko lako. 11Watu wake wote wanalia kwa uchungu
watafutapo chakula;
wanabadilisha hazina zao kwa chakula
ili waweze kuendelea kuishi.
“Tazama, Ee Bwana, ufikiri,
kwa maana nimedharauliwa.” 12“Je, si kitu kwenu, ninyi nyote mpitao kando?
Angalieni kote mwone.
Je, kuna maumivu kama maumivu yangu
yale yaliyotiwa juu yangu,
yale Bwana aliyoyaleta juu yangu
katika siku ya hasira yake kali?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.