Yona 2:3
Jonah 2:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ulinitupa kwenye kilindi, ndani kabisa ya moyo wa bahari, mikondo ya maji ilinizunguka, mawimbi yako yote na viwimbi vilipita juu yangu.
Jonah 2:3 in English
Jonah 2:3 · Berean Standard Bible
For You cast me into the deep, into the heart of the seas, and the current swirled about me; all Your breakers and waves swept over me.
Context
1Akiwa ndani ya tumbo la nyangumi, Yona alimwomba Bwana Mungu wake. 2Akasema:
“Katika shida yangu nalimwita Bwana,
naye akanijibu.
Kutoka kina cha kaburi* niliomba msaada,
nawe ukasikiliza kilio changu. 3Ulinitupa kwenye kilindi,
ndani kabisa ya moyo wa bahari,
mikondo ya maji ilinizunguka,
mawimbi yako yote na viwimbi
vilipita juu yangu. 4Nikasema, ‘Nimefukuziwa
mbali na uso wako,
hata hivyo nitatazama tena
kuelekea Hekalu lako takatifu.’ 5Maji yaliyonimeza yalinitisha,
kilindi kilinizunguka;
mwani* ulijisokota kichwani pangu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.