Yoeli 2:8
Joel 2:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hakuna anayemsukuma mwenzake; kila mmoja anakwenda mbele moja kwa moja. Wanapita katika vizuizi bila kuharibu safu zao.
Joel 2:8 in English
Joel 2:8 · Berean Standard Bible
They do not jostle one another; each proceeds in his path. They burst through the defenses, never breaking ranks.
Context
6Wanapoonekana, mataifa yanakuwa katika maumivu makuu;
kila uso unabadilika rangi. 7Wanashambulia kama wapiganaji wa vita;
wanapanda kuta kama askari.
Wote wanatembea katika safu,
hawapotoshi safu zao. 8Hakuna anayemsukuma mwenzake;
kila mmoja anakwenda mbele moja kwa moja.
Wanapita katika vizuizi
bila kuharibu safu zao. 9Wanaenda kasi kuingia mjini;
wanakimbia ukutani.
Wanaingia ndani ya nyumba;
kwa kuingilia madirishani kama wevi. 10Mbele yao dunia inatikisika,
anga linatetemeka,
jua na mwezi vinatiwa giza,
na nyota hazitoi mwanga wake tena.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.