Yoeli 2:10
Joel 2:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mbele yao dunia inatikisika, anga linatetemeka, jua na mwezi vinatiwa giza, na nyota hazitoi mwanga wake tena.
Joel 2:10 in English
Joel 2:10 · Berean Standard Bible
Before them the earth quakes; the heavens tremble. The sun and moon grow dark, and the stars lose their brightness.
Context
8Hakuna anayemsukuma mwenzake;
kila mmoja anakwenda mbele moja kwa moja.
Wanapita katika vizuizi
bila kuharibu safu zao. 9Wanaenda kasi kuingia mjini;
wanakimbia ukutani.
Wanaingia ndani ya nyumba;
kwa kuingilia madirishani kama wevi. 10Mbele yao dunia inatikisika,
anga linatetemeka,
jua na mwezi vinatiwa giza,
na nyota hazitoi mwanga wake tena. 11Bwana anatoa mshindo wa ngurumo
mbele ya jeshi lake;
majeshi yake hayana idadi,
ni wenye nguvu nyingi
wale ambao hutii agizo lake.
Siku ya Bwana ni kuu,
ni ya kutisha.
Ni nani anayeweza kuistahimili? 12“Hata sasa,” asema Bwana,
“nirudieni kwa mioyo yenu yote,
kwa kufunga, kwa kulia na kuomboleza.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.