Native Bible

Joel 2:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wanaonekana kama farasi; wanakwenda mbio kama askari wapanda farasi.

Joel 2:4 in English

Joel 2:4 · Berean Standard Bible

Their appearance is like that of horses, and they gallop like swift steeds.*

Context

2siku ya giza na huzuni, siku ya mawingu na utusitusi. Kama mapambazuko yasambaavyo toka upande huu wa milima hata upande mwingine jeshi kubwa na lenye nguvu linakuja. Jambo kama hili halijakuwepo tangu zamani wala halitakuwepo tena kamwe kwa vizazi vijavyo. 3Mbele yao moto unateketeza, nyuma yao miali ya moto inawaka kwa nguvu. Mbele yao nchi iko kama bustani ya Edeni, nyuma yao ni jangwa lisilofaa: hakuna kitu kinachowaepuka. 4Wanaonekana kama farasi; wanakwenda mbio kama askari wapanda farasi. 5Wanatoa sauti kama magari ya vita, wanaporukaruka juu ya vilele vya milima, kama mlio wa miali ya moto ilayo mabua, kama jeshi kubwa lililojipanga kwa ajili ya vita. 6Wanapoonekana, mataifa yanakuwa katika maumivu makuu; kila uso unabadilika rangi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.