Yoeli 2:26
Joel 2:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mtakuwa na wingi wa vyakula mpaka mshibe, na mtalisifu jina la Bwana Mungu wenu, ambaye amefanya maajabu kwa ajili yenu; kamwe watu wangu hawataaibishwa tena.
Joel 2:26 in English
Joel 2:26 · Berean Standard Bible
You will have plenty to eat, until you are satisfied. You will praise the name of the LORD your God, who has worked wonders for you. My people will never again be put to shame.
Context
24Sakafu za kupuria zitajaa nafaka,
mapipa yatafurika mvinyo mpya na mafuta. 25“Nitawalipa kwa ajili ya miaka ile iliyoliwa na nzige:
parare, madumadu na tunutu,
jeshi langu kubwa ambalo
nililituma katikati yenu. 26Mtakuwa na wingi wa vyakula mpaka mshibe,
na mtalisifu jina la Bwana Mungu wenu,
ambaye amefanya maajabu kwa ajili yenu;
kamwe watu wangu hawataaibishwa tena. 27Ndipo mtakapojua kwamba mimi niko katika Israeli
kwamba mimi ndimi Bwana Mungu wenu,
na kwamba hakuna mwingine;
kamwe watu wangu hawataaibika tena. 28“Hata itakuwa, baada ya hayo,
nitamimina Roho wangu juu ya wote wenye mwili.
Wana wenu na binti zenu watatabiri,
wazee wenu wataota ndoto,
na vijana wenu wataona maono.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.