Yoeli 2:24
Joel 2:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sakafu za kupuria zitajaa nafaka, mapipa yatafurika mvinyo mpya na mafuta.
Joel 2:24 in English
Joel 2:24 · Berean Standard Bible
The threshing floors will be full of grain, and the vats will overflow with new wine and oil.
Context
22Msiogope, enyi wanyama pori,
kwa kuwa mbuga za malisho yenu
zinarudia ubichi.
Miti nayo inazaa matunda,
mtini na mzabibu inatoa utajiri wake. 23Furahini, enyi watu wa Sayuni,
shangilieni katika Bwana Mungu wenu,
kwa kuwa amewapa mvua za vuli
kwa kipimo cha haki.
Anawapelekea mvua nyingi,
mvua ya vuli na ya masika, kama mwanzoni. 24Sakafu za kupuria zitajaa nafaka,
mapipa yatafurika mvinyo mpya na mafuta. 25“Nitawalipa kwa ajili ya miaka ile iliyoliwa na nzige:
parare, madumadu na tunutu,
jeshi langu kubwa ambalo
nililituma katikati yenu. 26Mtakuwa na wingi wa vyakula mpaka mshibe,
na mtalisifu jina la Bwana Mungu wenu,
ambaye amefanya maajabu kwa ajili yenu;
kamwe watu wangu hawataaibishwa tena.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.