Ayubu 9:26
Job 9:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Zinapita upesi kama mashua ya mafunjo, mfano wa tai ayashukiaye mawindo kwa ghafula.
Job 9:26 in English
Job 9:26 · Berean Standard Bible
They sweep by like boats of papyrus, like an eagle swooping down on its prey.
Context
24Wakati nchi inapoangukia mikononi mwa waovu,
yeye huwafunga macho mahakimu wake.
Kama si yeye, basi ni nani? 25“Siku zangu zapita mbio kuliko mkimbiaji;
zinapita upesi bila kuona furaha hata kidogo. 26Zinapita upesi kama mashua ya mafunjo,
mfano wa tai ayashukiaye mawindo kwa ghafula. 27Kama nikisema, ‘Nitayasahau malalamiko yangu,
nitabadili sura ya uso wangu na kutabasamu,’ 28bado ninahofia mateso yangu yote,
kwa kuwa ninajua hutanihesabu kuwa sina hatia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.