Native Bible

Job 8:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Je, hawatakufundisha na kukueleza? Je, hawataleta maneno kutoka kwenye kufahamu kwao?

Job 8:10 in English

Job 8:10 · Berean Standard Bible

Will they not teach you and tell you, and speak from their understanding?

Context

8“Ukaulize vizazi vilivyotangulia na uone baba zao walijifunza nini, 9kwa kuwa sisi tumezaliwa jana tu na hatujui lolote, nazo siku zetu duniani ni kama kivuli tu. 10Je, hawatakufundisha na kukueleza? Je, hawataleta maneno kutoka kwenye kufahamu kwao? 11Je, mafunjo yaweza kumea mahali pasipo na matope? Matete yaweza kustawi bila maji? 12Wakati bado yanaendelea kukua kabla ya kukatwa, hunyauka haraka kuliko majani mengine.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.