Ayubu 7:4
Job 7:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakati nilalapo ninawaza, ‘Itachukua muda gani kabla sijaamka?’ Usiku huwa mrefu, nami najigeuzageuza hadi mapambazuko.
Job 7:4 in English
Job 7:4 · Berean Standard Bible
When I lie down I think: ‘When will I get up?’ But the night drags on, and I toss and turn until dawn.
Context
2Kama mtumwa anavyovionea shauku vivuli vya jioni,
au mtu aliyeajiriwa anavyoungojea mshahara wake, 3ndivyo nilivyogawiwa miezi ya ubatili,
nami nimeandikiwa huzuni usiku hata usiku. 4Wakati nilalapo ninawaza, ‘Itachukua muda gani kabla sijaamka?’
Usiku huwa mrefu, nami najigeuzageuza hadi mapambazuko. 5Mwili wangu umevikwa mabuu na uchafu,
ngozi yangu imetumbuka na kutunga usaha. 6“Siku zangu zinapita upesi kuliko mtande wa kufuma,
nazo zinafikia mwisho wake bila matumaini.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.